Tom Emmer ajitoa kugombania uspika wa baraza la wawakilishi Marekani

Mbunge wa chama cha Repablikan, Tom Emmer, Jumanne amejitoa kugombea uspika wa baraza la wawakilishi la Marekani, ikiwa ni hatua nyingine inayowatatiza wabunge wanaopata wakati mgumu kwa wiki ya tatu kujaza nafasi hiyo ya juu katika majukumu ya serekali ya Marekani.

Nafasi ya spika imekuwa wazi toka Oktoba 3, wakati mbunge Kevin McCathy, alipojikuta akiwa wa kwanza katika historia ya Marekani kuondolewa katika nafasi ya uspika.

Wabunge wanane wa chama cha Republikan, walijiunga na Wademokrat 212 katika upigaji kura uliyeomuondoa McCathy.

Emmer amekuwa mwakilishi mwingine kujiondoa katika kundi la Warepublikan wanane baada ya kufanyika kura za siri mapema Jumanne.

Emmer, 62 alihudumu katika kundi la waliowengi, moja ya uongozi wa juu katika mkutano wa baraza la wawakilishi toka mwanzoni mwa mwaka huu.

Anawakilishi jimbo la magharibi kati la Minnesota, toka mwaka 2015.