Mbunge Tundu Lissu akamatwa Bungeni Dodoma

Tundu Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amekamatwa na polisi akiwa nje ya Bunge mjini Dodoma leo.

Taarifa ya Chama chake cha Chadema imesema hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Wakili wake Peter Kibatala ameiambia idhaa ya Kiswahili VOA askari polisi kadhaa wakiongozwa na aliyetambuliwa kama mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dodoma.

Hata hivyo wakili wake amedai kuwa mteja wake hakuonyeshwa hati inayotoa amri akamatwe.

Wakili huyo amesema kuwa aliwasiliana naye mara baada ya kukamatwa.