Timu ya WHO imeitembelea China na maeneo ya chanzo cha Corona

Timu ya WHO ikichunguza kiini cha COVID katika eneo la Wuhan huko China, January 30, 2021.

Wanasayansi hao wametembelea soko la samaki la Huanan ambalo lilihusishwa na kesi za COVID-19 na angalau moja ya hospitali huko Wuhan ambayo ilitoa huduma kwa baadhi ya wagonjwa wa kwanza wa Corona. COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona

Timu ya wanasayansi wa shirika la afya Duniani-WHO inayochunguza chanzo cha virusi vya Corona ambacho kiliibuka kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019 wametembelea Jumatatu kituo cha kudhibiti magonjwa mkoani humo ambacho kilikuwa na jukumu muhimu katika usimamizi wa mlipuko huo.

China haikutoa maelezo yeyote kuhusu ziara ya timu hiyo kwenda kituo cha kudhibiti magonjwa cha mkoa wa Hubei. Mmoja wa wanasayansi katika timu hiyo Peter Daszak amewaambia waandishi wa habari kuwa mkutano ulikuwa mzuri na uliozaa matunda.

Tangu timu ya WHO ilipowasili mwezi uliopita wanasayansi hao pia wametembelea soko la samaki la Huanan, ambalo lilihusishwa na kesi za COVID-19 na angalau moja ya hospitali huko Wuhan ambayo ilitoa huduma kwa baadhi ya wagonjwa wa kwanza wa Corona. COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.