Katika michuano ya ligi ya klabu bingwa ya ligi ya mpira wa kikapu barani Afrika kanda ya Nile katika uwanja wa Hassan Mostapha indoor Complex timu za Petro de Luanda ya Angola na Ferroviario da Beira ya Msumbiji walipambana Jumamosi.
Uongozi mkubwa zaidi wa Petro katika mchezo ulikuja katika kota ya 3 walipokuwa mbele kwa pointi 18.
Pointi tatu nyingine zinapachikwa wakati Majok wa Petro anapompasia Bastos na kuendeleza uongozi wao.
Petro walikuwa mbele kwa muda mwingi wa mchezo huo, kuibuka washindi dhidi ya vijana wa Beira kwa jumla ya pointi 101 kwa 76.
Na katika mchezo mwingine timu ya Afrika Mashariki katika kanda ya Nile City Oilers ya Uganda ilijikuta haina bahari baada ya kupoteza mchezo wake wa pili dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Oilers watajilaumu wenyewe katika mchezo huo baada ya kukosa kuingiza pointi tatu mwisho ni mwa mchezo ambayo ingeweza kluwapa ushindi.
Hadi mwisho wa mchezo uliokuwa na ushindani mkali AlAhly ya Misri waliibuka na ushindi kwa jumla ya pointi 72 kwa 70 kujipatia ushindi wao wa pili wa kanda ya Nile.
Na katika mechi za Jumapili timu ya SLAC ya Guinea ilipambana na Ferroviario da Beira ya Msumbiji.
Katika mchezo huo Beira ilifanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza wa kwanza wa kanda ya Nile kwa jumla ya pointi 109 kwa 97.
Na katika mchezo wa mwisho siku ya Jumapili Petro de Luanda ya Angola ilikwaana na Cape Town Tigers ya Afrika Kusini.
Vijana wa Petro wa Angola walionyesha mapema uwezo na nia ya ushindi
Petro walitawala mchezo wote na kupata ushindi kwa jumla ya pointi 87 kwa 48, na kupata ushindi wao wa tatu katika kanda ya Nile mpaka sasa.