Rama mwishoni mwa wiki alisema kuwa TikTok itafungwa nchini humo kwa muda wa mwaka mmoja, akiilaumu kwa kuchochea ghasia pamoja na uonevu, na hasa dhidi ya watoto.
Mamlaka zimefanya mikutano 1,300 na waalimu pamoja na wazazi tangu kisa cha kuchomwa kichu cha Novemba dhidi ya kijana mmoja, baada ya kubishana na mwenzake kupitia app hiyo. Asilimia 90 yao walipitisha kuwa TikTok ipigwe marufuku nchini humo.
Kufuatia uamuzi huo TikTok imeomba ufafanuzi wa dharura kutoka kwa serikali ya Ablania, kuhusu tukio hilo la uchomaji kisu. Kampuni hiyo imesema kuwa haikupata ushahidi wowote kwamba wahusika kwenye tukio hilo walikuwa na akaunti za TikTok, na kwamba ripoti kadhaa zimedhibitisha kuwa video zilizopelekea tukio hilo zilisambazwa kupitia majukwaa mengine, na wala siyo TikTok.