Theluji yaathiri utendaji kazi Marekani

Hali ya theruji Marekani

Dhoruba ya theluji, barafu, upepo na kushuka kwa viwango vya hali ya hewa nchini Marekani kumesababisha hali ya hatari.

Hali ya theruji imeathiri usafiri katika majimbo ya kati na kusini mpaka mashariki mapema Jumatatu, na kupelekea shule na ofisi za serikali kufungwa katika majimbo kadhaa.

Theluji na barafu zilifunika barabara kote huko Kansas, Nebraska magharibi na sehemu za Indiana, ambako Kikosi cha Ulinzi cha Taifa katika jimbo kilikuwa kikifanya kazi kuwasaidia wenye magari. Takriban nchi 8 za theluji zilitarajiwa kuanguka, pamoja na upepo mkali wa kasi ya kilometa 72 kwa saa.

Shule nyingi zimefungwa leo Jumatatu. Katika wilaya za Indiana, Virginia na Kentucky ilitangazwa kufutwa na kuchelewa kufunguliwa shule hadi mchana. Madarasa pia yalifutwa katika jimbo la Maryland ambako Gavana Wes Moore alitangaza hali ya dharura jana Jumapili na kutangaza kuwa serikali ya jimbo imefungwa leo Jumatatu.

Mwishoni mwa wiki, takriban wenye magari 600 walikuwa wamekwama huko Missouri maafisa wamesema. Mamia ya ajali za gari zimeripotiwa huko Virginia, Indiana, Kansas na Kentucky.

Hali mbaya ya hewa pia imesebabisha majimbo kadhaa kufuta safari za ndege kutokana na theluji iliyoanguka na inayoendelea kuanguka.