Theresa May kujiuluzu uwaziri mkuu Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akitangaza kuwa atawachia wadhifa huo kuanzia June 7, 2019.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema hivi leo Ijumaa kuwa atajiuzulu wadhifa huo, na mara moja kuchochea kuanza kwa ushindani ambao utamuingiza kiongozi mpya madarakani ambaye huenda akaongoza juhudi mpya za kupatikana kwa muafaka wa Brexit ili kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Kuondoka kwake kutazidisha mzozo wa Brexit na kiongozi mpya huenda akataka maamuzi yanayoweza kuleta mgawanyiko, na kuongeza makabiliano na Umoja wa Ulaya na pengine uchaguzi wa ghafla wa bunge ambao haukutarajiwa.

May ametangaza ratiba ya kuondoka kwake kuwa itaanza na kujiuzulu kama mkuu wa chama cha Conservative June 7, hatua itakayofuatiwa na uchaguzi wa uongozi katika chama hicho.

Sauti yake ikiwa inatetemeka na imejaa hisia, May ambaye alikabiliwa na mizozo na shutuma kwa kushindwa kwake kubuni muafaka wa makubaliano ya Brexit ambayo bunge yangeyaidhinisha, amesema hana kinyongo.

“Muda mfupi nitaondoka katika nafasi hii ambaye imekuwa ni heshima kubwa kwangu kuishika. Nikiwa mwanamke wa pili waziri mkuu lakini kwa hakika sitakuwa wa mwisho. Nafanya hivi bila ya nia mbaya lakini kwa heshima na shukran kubwa sana ya kuweza kupata fursa ya kuitumikia nchi hii ninayoipenda.”

May ambaye kuna kipindi hakuwa mfuasi mkubwa wa unachama wa EU, alishinda wadhifa wa juu katikati ya mivutano ambayo ilifuatia kura ya Brexit mwaka 2016, na sasa anaachia uongozi huku ahadi zake zikiwa ni kuiongoza Uingereza kutoka nje ya umoja huo na kuponya migawanyiko, jambo ambalo hakuweza kulifanikisha.

May anaiacha nchi ikiwa na mgawanyiko mkubwa na wanasiasa wakiwa wamekwama jinsi au lini kama wanataka kuondoka katika EU.

Washindani ambao huenda wakachukua nafasi ya May wote wanataka kuondoka katika makubaliano mazito ya kuondoka katika umoja huo, ingawaje EU imesema haitafanya mashauriano mengine ya mkataba wa kujitoa ambao ulifikiwa mwezi Novemba.

Wanasiasa kadhaa wametajwa kuwa huenda wakawania nafasi hiyo ya uwaziri mkuu wa Uingereza.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.