Jumatano tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 5.9 kwa kipimo cha Rikta lilipiga mashariki mwa nchi, liliangusha nguzo za simu na umeme na kusababisha maporomoko ya mawe na matope ambayo yameziba barabara za milimani.
Mohamed Amin Huzaifa, mkuu wa habari katika jimbo la Paktika lililoharibiwa vibaya, ameliambia shirika la habari la AFP leo kwamba kupata taarifa katika eneo hilo imekuwa vigumu sana kwa sababu ya mitandao mibaya.
Ameongeza kuwa hakuna taarifa mpya za idadi ya vifo kutoka kwenye eneo hilo.
Janga hilo limesababisha changamoto za kimkakati kwa serikali mpya ya Taliban nchini Afghanistan ambayo imejitenga yenyewe na sehemu kubwa ya dunia kwa utawala wenye msimamo mkali wa Kiislamu ambao unawakandamiza wanawake na wasichana.