Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania-TCRA imesitisha kurasa za mtandao wa kijami za kampuni moja ya vyombo vya habari nchini humo kwa madai ya kuchapisha maudhui yaliokatazwa na kuongeza kile ambacho makundi ya haki za binadamu yameeleza kuwa ni kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.
TCRA ilisema Jumatano imesitisha kwa muda leseni za maudhui ya mtandaoni kwa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kwa siku 30, inasema ilichapisha maudhui Oktoba Mosi ambayo yaliharibu taswira ya nchi.
Mwananchi Communication Ltd ilichapisha maudhui ya sauti hadi picha katika mitandao yake ya kijamii ambayo yamepigwa marufuku kutoka “Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni mwaka 2020,” mdhibiti alisema.
Maudhui hayo yamesababisha tafsiri mbaya kwa taifa ambapo yanaathiri na kuvuruga umoja, amani na umoja wa kitaifa.