Bunge la Ethiopia limemchagua waziri wa mambo ya nje Taye Atske-Selassie kuwa rais mpya wa nchi hiyo, nafasi ambayo kwa kiasi kikubwa haina nguvu nyingi serikalini.
Taye anachukua nafasi hiyo kutoka kwa rais Sahle-Work Zewde, ambaye amekuwa ofisini tangu mwaka 2018.
Bunge la Ethiopia humchagua rais na chama kinachotawala cha waziri mkuu kina idadi kubwa ya wabunge.
Kuchaguliwa kwake kumeidhinishwa wakati wa kikao cha bunge Jumatatu.
Taye ameapa kushiriki kikamilifu katika maswala ya amani katika pembe ya Afrika, hasa namna ya kutafuta suluhu ya vita vya Sudan.
Amesema kwamba Ethiopia vile vile itashirikiana na nchi jirani kuimarisha uhusiano.
Kulingana na shirika la habari la serikali ya Ethiopia, Taye amesema kwamba Ethiopia imesaini makubaliano na Somaliland kuhusu matumizi ya bahari ya Somaliland kwa shughuli za bandari.