Wamasai wa Loliondo wameishtumu serikali ya Tanzania kujaribu kuwaondoa kwa nguvu kwenye ardhi yao ili kuandaa utalii na mashindano ya uwindaji.
Lakini serikali ilitupilia mbali tuhuma hizo, ikidai kwamba inataka kulinda ardhi ya kilomita mraba 1,500 ili isiharibiwe na shughuli za binadamu. Inasema ni sehemu ndogo ya eneo ambalo linachukua kilomita mraba 4,000 karibu na mpaka wa Kenya.
Mvutano juu ya mradi huo ulisababisha kifo cha askari polisi mmoja wakati wa maandamano ya tarehe 10 mwezi huu, baada ya wafanyakazi kujitokeza na kuweka mipaka ili kutenganisha eneo la kulindwa.
“Kufuatia maelekezo ya waziri wa mambo ya ndani, tutaendesha operesheni kwa siku 10 dhidi ya wahamiaji haramu pembeni mwa Loliondo na wilaya ya Ngorongoro,” Kamishna mkuu wa idara ya uhamiaji, Anna Makakala, amesema Jumatano.