Membe asema yuko tayari kuwania urais Tanzania kupitia CCM

Bernard Membe

Anataka Kamati Kuu ya chama tawala CCM itoe tamko kuhusu uanachama wake

Your browser doesn’t support HTML5

Membe kujaza kugombea urais Jumatatu iwapo Kamati Kuu ya CCM itamjibu


Waziri wa zamani wa mambo ya nje Tanzania Bernard Membe anasema yuko tayari kuingia katika kinyang’anyiro cha ugombea urais kupitia chama tawala cha CCM mwaka huu endapo Kamati Kuu ya chama hicho itatoa tamko kwamba hajafutiwa uanachama wake.

Your browser doesn’t support HTML5

Membe ataka Kamati Kuu ya CCM itoe tamko juu ya uanachama wake


Akizungumza Jumamosi mkoani Lindi, kusini mwa Tanzania, Membe alisema anahitaji Kamati Kuu itoe tamko kuhusu uanachama wake na uhuru wake wa kuingia katika kinyang’anyiro ili asiwekewe vikwazo katika hatua za kuchukua fomu na kutafuta wadhamini endapo atatangaza nia bila uwazi kuhusu msimamo wa Kamati ya Kuu juu yake.

Mpaka sasa ni Rais John Pombe Magufuli peke yake ambaye amechukua fomu kuwania urais kwa tiketi ya CCM, akiwa anawania awamu ya pili ya uongozi. Endapo Membe ataingia katika kinyang’anyiro hicho itakuwa jambo la nadra kwa rais aliyeko madarakani Tanzania kupata changamoto ndani ya chama chake wakati anawania awamu ya pili.

Membe amelazimika kutoa matamshi hayo Jumamosi kutokana na kiwingu kwamba huenda amevuliwa uanachama wa CCM kufuatia kashfa ya mwaka 2019 ambayo ilihusisha pia wanachama wengine waandamizi wa CCM waliosikika katika mazungumzo ya simu wakimsema mwenyekiti wa chama hicho Rais Magufuli.

Wenzake katika kashfa hiyo makatibu wakuu wa zamani Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na aliyekuwa katibu mwenezi Nape Nnauye walipewa onyo na Kamati ya Maadili ya chama na baadaye wakaomba samahani kwa mwenyekiti Magufuli.

Tangu wakati huo Membe amekuwa katika mvutano na Kamati Kuu ya CCM na kusababisha sintofahamu kwa wengi endapo amefutwa uanachama ama la.

Membe alifafanua kwamba kulingana na anavyofahamu taratibu za CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) peke yake ndio yenye mamlaka ya kumfukuzu au kumrudishia mjumbe uanachama wake.

Kwa maelezo yake hata kama Kamati ya Maadili na Kamati Kuu za CCM zimependekeza Membe afukuzwe uanachana ni NEC pekee inayoweza kufanya hivyo na kikao chake hakijafanyika hadi mwezi Julai.

Membe alisema pia alipotokea mbele ya Kamati ya Maadili mwanzoni mwa mwaka huu kamati hiyo ilimhakikishia kwamba sio kosa kwake kutaka kuwania ugombea urais kupitia chama cha CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.

Your browser doesn’t support HTML5

Membe awapongeza wana CCM Zanzibar na wapinzaniTanzania bara


Katika hotuba yake Membe pia aliwasifu wanachama cha CCM Zanzibar na wanachama wa vyama vya upinzani kwa kujitokeza kwa wingi katika vinyang’anyiro vya ugombea ndani ya vyama vyao akisema hicho ni kielelezo cha demokrasia iliyochangamka.