Watanzania wanatoa maoni yanayo tofautiania juu ya miaka 49 uhuru. Kufuatana na wachambuzi wa mambo kuna baadhi wanao amaini Uhuru umewaletea uwezo wa kujitawala, baadhi ya manedeleo vijijini lakini wengine walokua na tamaa ya maendeleo ya haraka wangali hawajaridhika.
Mhadhir wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam Dk.Bashiru Ally ameiambia Sauti ya Amerika kwamba thamini ni ya mchanganyiko na changamoto kutokana na vile maendeleo ya wananchi hayajapatikana baado.
Kwa upande wake akizungumza na Sauti ya Amerika Profesa Ibrahim Lipumba, mchumi, kiongozi wa upinzani anasema kuna changmoto kubwa kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama wengiu walivyotarajia waliponyakua uhuru hapo Disemba 9 1961.