TAKUKURU kuwashitaki watuhumiwa, Tanzania.

Rais John Magufuli wa Tanzania.

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania, TAKUKURU, imebainisha kuwa inashughulikia kukamilisha kesi kubwa za Rushwa 36, zinazowahusu watuhumiwa wenye ushawishi na hadhi kubwa nchini .

Your browser doesn’t support HTML5

Ufisadi Tanzania

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amezitaja miongoni mwa kesi hizo, kuwa ni za ukwepaji kodi wa Kampuni ya mafuta ya Lake Oil, ambapo hiyo inatuhumiwa kuisababishia serikali hasara ya takribani fedha za kitanzania shilingi Bilion 8.5


Wakati huo huo ,mkuu wa Mashtaka nchini anasuburiwa kutoa kibali cha kuwafikisha watuhumiwa wote waliobainika kujihusisha na matendo ya Rushwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni za Ununuzi wa umma kwenye kesi ya mabehewa ya kokoto ya shirika la Reli nchini ,TRL.