Magufuli achaguliwa rais mpya Tanzania

Wafuasi wa CCM wakishangilia ushindi wa John Magufuli Tanzania

Tume ya uchaguzi Tanzania imetangaza rasmi kuwa John Magufuli wa chama tawala cha CCM ameshinda uchaguzi wan chi hiyo baada ya kupata asilimia 58 ya kura zote dhidi ya mgombea wa upinzani Edward Lowassa wa Ukawa aliyepata asilimia 40 ya kura.

Your browser doesn’t support HTML5

Magufuli atangazwa mshindi

Lowassa alipinga matokeo hayo kabla hayajatolewa rasmi na inaripotiwa ameyakataa tena na kuishutumu tume kwa kujaribu “kuiba haki ya kidemokrasia ya Watanzania.”

Your browser doesn’t support HTML5

Ukawa wapinga matokeo

Lowassa amesema kuwa yeye ndiye aliyeshinda katika uchaguzi mkuu wa Jumapili kwa kupata zaidi ya kura milioni 10 ikiwa ni sawa na asilimia 62.

Rais Kikwete anaondoka madarakani baada ya miaka 10.

Watanzania walipiga kura Jumapili Oktoba 25 kuchagua rais mpya wa Jamhuri ya muungano, rais wa Zanzibar, wajumbe wa bunge la muungano na baraza la wawakilishi Zanzibar.

Kipindi cha matokeo kimekuwa na vuta nikivute nyingi na Jumanne mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha alitangaza kuwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar yamefutwa.

Makundi ya ndani ya nchi na ya kimataifa mpaka sasa yanaiwekea shinikizo tume hiyo kubadili uamuzi wake na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kama yalivyo.

Kufutwa kwa matokeo hayo kunaathiri matokeo ya uchaguzi wa rais Zanzibar na wajumbe wa baraza la wawakilishi.