Taliban wa Pakistan wafanya shambulizi la kigaidi Pakistan

Serekali ya kaskazini magharibi mwa Pakistani, Alhamisi imesema wanamgambo wamefanya shambulizi la bunduki na bomu kwenye kituo cha polisi, na kuwauwa wanajeshi watatu wa kikosi cha usalama.

Kundi lililopigwa marufuku la Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP), linalo julikana kama Taliban wa Pakistani, lilidai kuhusika na shambulizi hilo baya la usiku katika wilaya ya Khyber, inayopakana na Afghanistan.

Mkuu wa polisi wa wilaya, Imran Khan, aliwaambia wanahabari kwamba takriban wanamgambo wanne waliokuwa na silaha nzito, ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, walivamia majengo kwa kile alichosema kuwa ni mashambulizi yaliyoratibiwa na kuwasababishia hasara.

TTP ilidai katika taarifa yake kwamba mshambuliaji pekee wa kujitoa mhanga ndiye aliyehusika na uvamizi wa kituo cha polisi.