Ripoti kutoka Iran zinasema waandamanaji hao kwa mara nyingine tena walipambana na vikosi vya usalama Alhamisi katika eneo lililo karibu na mji mkuu, wakiripotiwa kuwaua au kuwajeruhi wanachama wa vikosi vya usalama.
Maandamano nchini Iran yamezuka karibu kila siku tangu Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wa maadili wa nchi hiyo.
Wachambuzi wanasema maandamano ya kila siku yamekuwa baadhi ya changamoto kubwa kwa Jamhuri hiyo ya Kiislamu katika historia yake.
Mapigano ya Alhamisi yalikuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika katika mji wa Karaj, nje kidogo ya Tehran, kuadhimisha siku ya 40 tangu kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Hadis Najafi mwenye umri wa miaka 22, mmoja wa wanawake vijana kadhaa waliouawa wakati wa maandamano