Tajiri Bloomberg ajiondoa kinyang'anyiro cha uchaguzi, amuunga mkono Biden

Meya wa zamani Mike Bloomberg

Mgombea aliyekuwa anawania uteuzi wa chama cha Democratic kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Marekani, tajiri Michael Bloomberg, ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kufanya vibaya katika uchaguzi wa awali Jumanne.

Bloomberg, ambaye hakupata mjumbe yeyote katika uchaguzi wa jana maarufu kama "Super Tuesday," ametangaza kumuunga mkono aliyekuwa Makamu wa Rais Joe Biden.

Bloomberg aliyeingia katika kinyang’anyiro hicho miezi mitatu iliyopita na kutumia dola nusu bilioni katika kampeni, amesema amejiondoa kwenye kinyang’anyiro ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya mgombea wa chama cha Democratic kumshinda Rais Donald Trump katika uchaguzi wa Novemba 2020.

Aliyekuwa Makam wa Rais Joe Biden amepata ushindi mkubwa wa majimbo tisa kati ya 14, katika uchaguzi wa Jumanne, akifuatiwa na seneta Bernie Sanders.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.