Sydney yatangaza kupitia janga la asili

Serekali ya Sydney Jumamosi imetangaza janga la asili katika sehemu za mashariki mwa Australia ambako upepo umeangusha miti na kukata umeme kwa maelfu ya nyumba.

Mvua kubwa, radi na upepo wenye kasi ya kilomita 100 kwa saa uliishambulia Sydney na maeneo mengine ya New South Wales toka Jumatano.

Huku njia nyingi za umeme zikiwa zimekatwa, takriban nyumba 30,000 zilikosa umeme Jumamosi, kiwango kikishuka kutoka nyumba zaidi ya 260,000, amesema waziri wa huduma za dharura wa jimbo hilo, Jihad Dib.

Amewaambia wanahabari kwamba tukio hilo lime athiri jimbo zima.

Idara ya huduma za dharura ilishughulikia zaidi ya matukio 7,000 karibu na New South Wales, amesema. Maafa yametangazwa hadi sasa katika maeneo matatu ya serikali za mitaa, na kumefunguliwa msaada kwa watu wanaotafuta makazi ya dharura, vitu muhimu, ukarabati na usafishaji.