Mabalozi wa nchi hizo mbili wameasilisha rasmi maombi ya nchi hizo katika makao makuu ya Nato.
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema kwamba hatua hiyo ni ya kihistoria na ambayo inastahili kukubaliwa.
Hatua ya kuidhinisha maombi uanachama wa mataifa hayo mawili huend aikachukua karibu mwaka mzima, ambapo mabunge ya nchi wanachama 30 yatajadili maombi hayo.
Uturuki imewashangaza washirika wake kwa kusema kwamba haijaridhishwa na maombi ya wanachama wapya hasa kutokana na kuwakubali wapiganaji wa Kikurdi kawenye ardhi yake.
Stoltenberg amesema kwamba maswala yeye utata yanaweza kuajdiliwa huku Marekani ikieleza matumaini kwamba maombi ya nchi hizo yatakubaliwa.
Finland, na Sweden zinapakana na Russia.
Endapo maombi hayo yatakubaliwa, muungano wa NATO utakuwa na udhibithi wa pwani nzima ya bahari ya Baltic.