Sunak aahidi kuisaidia Ukraine katika mkutano wa kikosi cha pamoja cha JEF kinachoongozwa na Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Viongozi wa nchi Kumi za kusini mwa Ulaya Jumatatu wamesema wataendelea kuisaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa kivita wa Russia wakati wakifanya mkutano wa kikosi cha pamoja kinachoongozwa na Uingereza – JEF huko Riga, nchini Latvia.

Viongozi wa nchi Kumi za kusini mwa Ulaya Jumatatu wamesema wataendelea kuisaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa kivita wa Russia wakati wakifanya mkutano wa kikosi cha pamoja kinachoongozwa na Uingereza – JEF huko Riga, nchini Latvia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliwaomba viongozi kwa njia ya video kumpatia mifumo mbalimbali ya silaha ili kumaliza mzozo mbaya zaidi barani Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alimshukuru Zelenskyy kwa kuelezea kuhusu msaada zaidi unaohitajiwa na Ukraine na akasema viongozi watajadiliana jinsi ya kuupeleka.

Akizungumza mbele ya Mkutano huo waziri wa ulinzi wa Uholanzi Kajsa Ollongren alisema uungwaji mkono wa nchi hizo 10 utaendelea kwa muda mrefu .

Kwa upande wake Sunak aliwaomba washirika wengine wa Ulaya kaskazini pia kutoa msaada katika vita hivyo akisisitiza kwamba “ usalama wao ni usalama wetu”.

Waziri Mkuu wa Uingereza: “ Nadhani pili kama Krisjanis Karisn Waziri Mkuu wa Latvia lazima tuwe wazi kwamba wito wowote wa upande mmoja wa kusitisha mapigano na Russia hauna maana kabisa katika muktadha wa sasa. Nadhani itakuwa wito wa uongo. Utatumiwa na Russia kujipanga, kuongeza nguvu vikosi vyao, na mpaka wamejiondoa kutoka eneo lililotekwa hakutakuwa na mazungumzo ya kweli. Lakini kitu tunachoweza kufanya ni kufikiria kuhusu muda huo sasa .kufikia kitu tunachoweza kufanya kuhakikisha usalama.”

Kikosi cha pamoja cha JEF kinaleta pamoja vikosi vingine kutoka nchi 10 ikiwemo mataifa ya kaskazinimashariki mwa ulaya na wameona umuhimu wake ukiongezeka tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine mwezi Februari.