Sudan yamuita balozi wake kutoka Ethiopia huku mahusiano yakizorota

Waethiopia wavuka mpaka kwenda kutafuta hifadhi katika jimbo la Kassala nchini Sudan. Picha na Reuters.

Sudan imemuita balozi wake kutoka nchi jirani ya Ethiopia leo Jumapili, ikiwa amefadhaishwa na msimamo wa maafisa wa Ethiopia, ambao walisema wanakataa ombi la Sudan, la kuwa mpatanishi katika mzozo unaoendelea, kwenye jimbo la Kaskazini mwa nchi hiyo la Tigray

"Ethiopia itaimarisha hali yake ikiwa itazingatia kile Sudan inaweza kufanya .. badala ya kukataa kabisa juhudi zake zote," ilisema taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Sudsan.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumatano juu ya mzozo katika jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia, ambao umesababisha kuwepo kwa wakimbizi wapatao 53,400 tangu mwishoni mwa mwaka 2020.

Ombi la Hamdok la kutaka kuwa mpatanishi limejiri wakati wa muhula wake kama mwenyekiti wa IGAD, kikundi cha kieneo, ambacho kinajumuisha Kenya, Ethiopia, Uganda, Djibouti, Sudan, Sudan Kusini, Uganda na Somalia, ilisema taarifa hiyo.