Sudan yahofiwa kufikia janga la njaa

Sudan imekuwa kitovu cha vita kwa muda wa mwaka mmoja sasa, ambayo imetokana na kuhasimiana kati ya jeshi na vikosi vya akiba vya RSF.

Mzozo huo umefunikwa na vita kati ya Israel na Hamas katika ukanda wa Gaza.

Kutonaka na hilo wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu wanaonya Sudan sasa inaelekea kwenye janga la njaa, na uwezekano wa vifo vya watu wengi katika miezi ijayo.

Miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa chakula imesambaratika na mashirika ya misaada hayawezi kufikia katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Wakati huo huo, mzozo huo umeleta taarifa nyingi za ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji, watu kuhama na ubakaji, hasa katika eneo la mji mkuu na eneo la magharibi la Darfur.