Sudan Kusini itaanza tena kuzalisha kwa wingi mafuta ghafi

Maeneo ya visima vya mafuta

Uzalishaji huo unatarajiwa kuongezeka kufikia mapipa 270,000 kwa siku ifikapo mwishoni mwa mwaka huu waziri wa mafuta wa Sudan Kusini Ezekiel Gatkuoth aliliambia shirika la habari la Reuters.

Sudan Kusini itaanza tena kuzalisha zaidi ya mapipa 350,000 ya mafuta ghafi kwa siku ifikapo kati kati yam waka 2020 ongezeko kutoka kiwango cha sasa cha zaidi ya mapipa 140,000 kwa siku alisema waziri wa mafuta nchini humo Ezekiel Lul Gatkuoth.

Uzalishaji unatarajiwa kuongezeka kufikia mapipa 270,000 kwa siku ifikapo mwishoni mwa mwaka huu Gatkuoth aliliambia shirika la habari la Reuters. Alikuwa akizungumza pembeni ya mkutano wa Petrotech katika mji mkuu wa India, New Delhi.

Taifa hilo changa duniani ambalo lilijitenga kutoka Sudan mwaka 2011 moja ya hazina yake kubwa sana ni mafuta ghafi katika mataifa ya Afrika, kusini mwa Sahara na ni theluthi moja pekee ya mafuta yake ndio yamekuwa yakichunguzwa.

Sudan Kusini imepoteza visima vyake vingi vya mafuta kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilizuka miaka miwili iliyopita baada ya kujipatia uhuru wake.