Umoja wa mataifa ulishindwa kulinda raia na wafanyakazi wa huduma-Uchunguzi huru

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. (AP Photo/Osamu Honda)

Uchunguzi huru kuhusiana na mapigano makali ya Julai nchini Sudan Kusini umekamilisha ripoti yake na kueleza kwamba jeshi la Umoja wa mataifa na ofisi ya wafanyakazi wake walishindwa kulinda raia na wafanyakazi wa huduma.

Uchunguzi huo ulioongozwa na Jenerali wa kiholanzi Patrick Cammaert umeonyesha kwamba ukosefu wa uongozi kwa upande wa viongozi wa juu wa umoja wa mataifa uliogubikwa na majibu yasio na athari yeyote kwa ghasia hizo kwa mujibu wa wachunguzi hao.

Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephanie Dujarric alisema katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameomba kamanda wa kikosi hicho kwenye ofisi ya Umoja wa mataifa Sudan Kusini aondolewe.

Msemaji huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba "Hayo ni moja ya mapendekezo yatakayochukuliwa hatua mara moja". Mengine yatangazwa kwa mpangilio maalum .