Fainali za kombe la dunia: US vs Japan
Wachezaji wa Japan wakiliwazana baada ya kupoteza mechi ya fainali.
Mashabiki wakifuatilia mechi hiyo katika televisheni kutoka National Harbor, Maryland
Mashabiki wa Japan wakiwa hawaamini macho yao wakati wanafuatilia mechi hiyo katika televisheni.
Timu ya Marekani wakiwa wanasherehekea na kikombe baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Japan.
Mashabiki wa Marekani wakiwa wamejipaka rangi za bendera ya taifa usoni kabla ya mechi.
Golikipa wa Japan Ayumi Kaihori akila nyasi huku mpira ukitinga langoni katika bao la nne la Marekani
Golikipa wa Marekani Hope Solo akikumbatiana na Carli Llyod baada ya kufunga bao lake la tatu dhidi ya Japan.
Golikipa wa Marekani Hope Solo akipanchi moja ya hatari hatari katika goli lake.
Mchezaji wa Marekani Alexi Morgan akiwa amejifunika bendera ya Marekani baada ya ushindi dhidi ya Japan.
Wachezaji wa Marekani wakipongezana baada ya ushindi wao wa kishindo dhidi ya Japan.
Megan Rapinoe na Sydney Laroux wa Marekani wakiwa wamejawa na furaha baada ya ushindi wao.
Wachezaji wa Marekani wakifurahia kombe la dunia
Wachezaji wa Marekani wanazunguka uwanja kuwasalimu mashabiki kwa kuwaunga mkono.
Golikipa wa Japan Ayumi Kaihori anajaribu kwa juhudi zote kuokoa goli lakini ni kazi bure.
Mchezaji wa Japan akijaribu kuwatoka walinzi wa Marekani wanaomwangalia kwa makini.