Moses Wentan’ugula aliwambia wabunge Jumanne kuwa lazima waheshimu sheria za mavazi za bunge, akikemea “mitindo inayoibuka ambayo sasa inatishia kanuni za mavazi za bunge.”
Amesema kile kinachoitwa suti aliyokuwa akipenda kuvaa hayati rais wa Zambia Kenneth Kaunda, limepigwa marufuku pia, pamoja na mavazi ya kitamaduni yasiyofaa.
Ruto huvaa mara nyingi suti za kawaida, lakini vazi la Kaunda sasa ndilo vazi lake analolipenda, na alilivaa wakati wa ziara ya Mfalme Charles wa tatu mapema mwezi huu.
Kulingana na kanuni za Spika, “vazi linalofaa kwa wanaume ni kanzu, kola, tai, shati la mikono mirefu, suruali ndefu, soksi na viatu.”
Kwa wanawake, sketi, na nguo lazima iwe chini ya goti na juu ya mikono, isiyokuwa na mikono ni marufuku.