Spika Pelosi wa Marekani asema Taiwan kutotengwa

Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi akiwa na rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen.

Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, Jumatano amesema ujumbe wa wawakilishi unaotembelea Taiwan unatoa ujumbe wa wazi kwamba Taiwan haito-telekezwa.

Amesema kwa sasa ushirika wa Taiwan, na Marekani, ni muhimu na ndio ujumbe ambao wameubeba.

Aligusia muswada mpya uliopitishwa wa kuongeza uzalishaji katika viwanda na kuisaidia Marekani kushindana na makampuni ya China.

Pelosi aliliambia bunge la Taiwan kwamba mswaada huo unatoa fursa kubwa kwa ushirikiano baina ya Taiwan na Marekani.

China imeeleza kupinga kwake ziara ya spika Pelosi, ikitahadharisha kuwa ni ukiukwaji usio kubalika wa kile inachokiona kuwa himaya yake katika kisiwa chenye utawala wake binafsi.