Somalia yapeleka maelfu ya wanajeshi nchi jirani kwa mafunzo

Serekali ya Somalia imepeleka maelfu ya wanajeshi wapya iliyo waandikisha katika mataifa ya jirani kwa ajili ya mafunzo.

Hatua hiyo ni koboresha jeshi katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabab, kwa mujibu wa mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa Somalia.

Katika mahojiano maalumu na VOA, mshauri huyo Hussein Sheikh-Ali, amesema Somalia imepeleka wanajeshi 3,000 kwa kila nchi za Eritrea na Uganda katika wiki kadhaa zilizopita.

Amesema kwamba wanajeshi zaidi 6,000 watakao andikishwa watapelekwa Ethiopia na Misri.

Ameiambia VOA kwamba wanataka kuwa wanajeshi 15,000 walio tayari katika mwaka huu wa 2023.

Mazungumzo yake na VOA yalikuwa ya ana kwa ana akiwa jijini Washington ambapo alikutana na maafisa wa Marekani ili kutafuta uungwaji mkozo zaidi kwa Somalia.