Soko la hisa la Tehran lashuka

Soko la hisa la Tehran, lilishuka kwa siku ya pili ya mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas, huku thamani ya jumla ikishuka kwa takriban pointi 51,000.

Kulingana na shirika la habari la ISNA makampuni mashuhuri, ikiwa ni pamoja na viwanda vya petroli vya ghuba ya Uajemi, usafishaji wa mafuta ya Esfahan, Kampuni ya maendeleo ya mafuta na gesi ya Parsian, usafishaji wa mafuta ya Bandar Abbas, na Mapna Group, yalikuwa mstari wa mbele katika bishara kwenye soko la hisa hata hivyo zote zilishuka Jumapili.

Kwa ujumla thamani ya masoko ilishuka kwa pointi 659, na kufungwa ikiwa na vitengo 25,025.

Mchumi Siamak Ghasemi, alihusisha kushuka kwa soko la hisa na dalili ya wazi ya kuongezeka kwa hatari ya kimfumo nchini Iran.

Katika ujumbe wa mtandao wa X zamani Twitter, alisema kuwa mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel na kuanza kwa mzozo mpya ni hatari kubwa zaidi kiuchumi na kimfumo nchini Iran, na pengine mashariki ya kati kwa mwaka huu.