Makumbusho ya Wamarekani Weusi yafunguliwa, Washington

Mke wa rais Barack Obama, Michelle akimkumbatia rais wa zamani George Bush aliyewezesha ujenzi wa jumba la makumbusho la wamarekani weusi

Jengo la makumbusho la Wamarekani weusi mjini Washington.

Kibanda cha mtumwa katika shamba la zamani la Point of Pines ni moja ya vielelezo katika Jumba la Makumbusho ya Historia na Utamaduni wa Wamarekani wenye asili ya Afrika, Washington, Sept. 14, 2016.

Picha hii iliyochukuliwa Julai 18, 2016, inaonyesha kibanda cha mtumwa kutoka Poolesville, Maryland.

Sanamu la Clara Brown, ambaye alizaliwa kama mtumwa huko Virginia katika miaka ya 1800.

Gauni la mmoja wa waanzilishi kampeni za haki za raia Rosa Parks nalo lipo katika maonyesho ya makumbusho haya mapya.

Fimbo ya kamba iliyokuwa ikitumiwa kuwaadhibu watumwa.

Aina ya minyororo iliyokuwa ikitumiwa kufunga watumwa.                          

Mnara wa saluti ya Black Power katika michezo ya Olimpiki ya Mexico mwaka 1968.