Maafisa wa wanyapori nchini Kenya wanasema Simba aliyetoka kutoka hifadhi ya wanyama ya taifa ya Nairobi alimshambulia mwanaume mmoja katika barabara yenye harakati nnyingi kwenye mji mkuu Nairobi Ijumaa.
Hii ni mara ya tatu chini ya kipindi cha mwezi mmoja kwamba Simba wametoroka kutoka kwenye hifadhi yao , na kusababisha taharuki kwa wakazi kwenye mji huo.
Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano hifadhi ya wanyamapori nchini Kenya Paul Udoto amesema Simba huyo mtoro alimkwaruza mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 68 na kwamba tabia hiyo ya wapita njia na waendesha magari wanastahili kulaumiwa.
Anasema “ mkusanyiko uliokuwepo dhidi ya simba huyo ulisababisha kelele, waendesha magari walikuwa wanapiga honi. Watu walikuwa wanapiga picha kwa ajili ya kurusha kwenye mtandao wa what’s up na mitandao mingine na Simba huyo aligadhabishwa na kumjeruhi mwanaume huyo”.
Hifadhi ya wanyama nchini Kenya ina karibu hekari 12,000 za ardhi. Maafisa wa hifadhi ya wanyama wamesema kutoroka wanyama sio jambo la kawaida lakini kinapata ushabiki mkubwa. Wanasema wakati wa majira ya mvua wanyama wanatabia ya kutembea nje ya eneo la hifadhi yao.
Hata hivyo msemaji wa hifadhi ya wanyama pori Udoto amesema watafanya uchunguzi dhidi ya matukio waliyoshuhudia katika miezi ya hivi karibuni ya wanyama kwenda katika maeneo ya makazi tofauti na njia zao.
Anasema “ ni jambo jipya hasa katika barabara ya Mombasa na Lang'ata ambazo zina harakati nyingi za watu na viwanda. Ni jambo tunalolifanyia uchunguzi kuona kwa undani nini kinasababisha Simba kwenda katika eneo hilo.
Mwezi Februari Simba wanne walitumia siku nzima wakitembea katika maeneo tofauti yenye makazi ya watu kwenye mji mkuu lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.