Wapiga kura nchini Ufaransa watamchagua rais katika duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika jumapili. Le Pen, mwenye sera kali dhidi ya uhamiaji, anawania kuwa kiongozi wa kwanza wa serikali kutoka mrengo wa kulia, mwenye siasa na msimamo mkali wa utawala. Ushindi wake huenda ukaleta wassiwasi mkubwa kote Ulaya.
Zimesalia siku mbili za kufanya kampeni. Alhamisi, Macron anakutana na wapiga kura kaskazini mwa Paris huku Le Pen, akifanya kampeni mjini Arras, kaskazini mwa nchi hiyo. Katika mjadala wa jumatano, ambao ulipeperushwa moja kwa moja na televisheni, Macro alilenga sana rekodi ya Le Pen, huku Le Pen akilenga sana utendakazi wa serikali ya Macron. Wakati Russia ikiwa imeivamia Ukraine, macro alizungumzia zaidi kuhusu hatua ya Le Pen kuchukua mkopo kutoka benki ya Russia kufadhili kampeni yake m waka 2017, na kumshutumu kwamba anategemea Russia na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.