Shughuli ya kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu nchini Marekani inaendelea kutafuta mshindi wa urais kati ya Rais Donald Trump na aliyekuwa makam wa rais Joe Biden.
Kufikia sasa, hakuna mgombea amefikisha idadi ya kura za wajumbe 270 zinazohitajika ili kutangazwa mshindi.
Chama cha rais Donald Trump cha Republican, kimetangaza kwamba kitawasilisha ombi mahakamani kutaka kura katika jimbo lenye ushindani la Wisconsin kurudiwa, baada ya kuwepo ishara kwamba Joe Biden atashinda jimbo hilo.
Chama hicho vile vile kinataka mahakama kuu kuingilia katika shughuli ya kuhesabu kura katika jimbo la Pennsylvania, akidai kwamba kuna udanganyifu ulikuwa unafanyika, bila kutoa Ushahidi wowote.
Shughuli ya kuhesabu kura inachukua mda mrefu kukamilika kutokana na idadi kubwa ya kura zilizopigwa kupitia njia ya posta.
Majimbo yenye ushindani mkubwa yanayosubiri matokeo ya kura ni Pamoja na Michigan, Wisconsin, North Carolina na Georgia.