Ameongeza kusema pia kwamba shirika lake linajitahidi kuongeza wasafiri ili kujikwamua kutokana na athari za janga la corona. Kilavika amesema kwamba baada ya miaka miwili ya kipindi kigumu kutokana na janga hilo , wanatarajia ongezeko la wasafiri mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ongezeko hilo litategemea kutokuwepo kufungwa kwa shughuli za kawaida kutokana na virusi vya Covid. Amesema pia kwamba anatumai uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti hautaathiri kipindi cha watalii kama ilivyo shuhudiwa katika miaka ya nyuma.
Shirika la ndege la Kenya ambalo pia linajulikana kama KQ linamilikiwa kwa asilimia 48.9 na serikali, na lilishuhudia kushuka kwa nusu ya mapato yake wakati wa janga la corona katika miaka miwili iliyopita. Mapato kutokana na wasafiri yaliongezeka kwa asilimia 21 mwaka jana, na kusaidia shirika hilo kupunguza hasara yake kwa theluthi 5 katika nusu ya kwanza ya mwaka jana. Licha ya hilo, hasara ya shilingi bilioni 11.5 bado ilipatikana katika kipindi hicho.