Shirika la ndege la Afrika kusini ambalo siku za hivi karibuni lilibinafsishwa katika juhudi za kuliokoa lisifilisike, Jumatano limesema litaanzisha tena safari zake mwezi Septemba.
Shirika hilo ambalo lilikuwa la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya shirika la ndege la Ethiopia, lilinusurika kwa miaka mingi kutokana na ruzuku za serikali, na lilisitisha safari zake hata kabla ya janga la Covid 19.
“Chini ya mwezi mmoja, ndege za shirika hilo zitaanza tena kuonekana kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo.
Awali,shirika hilo lilisema kuwa safari za ndani kutoka Johannesburg kuelekea Cape Town,pamoja na safari kwenye miji mingine ya Afrika kama Accra, Kinshasa, Harare, Lusaka na Maputo zitaanza karibuni.
Mwezi Juni, serikali ya Afrika Kusini iliuza asilimia 51 ya hisa zake katika shirika hilo kwa muungano na mashirika mengine ikiwemo mmiliki wa sasa wa shirika hilo, LIFT.