Shirika hilo la haki za binadamu lenye makao yake mjini Cairo (AOHR) limepongeza hatua ya Libya kuwapokea wahamiaji hao “waliopitia hali ngumu ya kibinadamu” kabla ya kuchukuliwa na walinzi wa mpakani wa Libya.
“Kulingana na walinzi wa mpakani wa Libya, wahamiaji 360 wakiwemo wanawake na watoto wanahitaji msaada wa haraka na matibabu, tawi la AOHR nchini Libya limesema, likiwasihi maafisa wa Libya “kuliruhusu shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM), kukutana na wahamiaji hao na kuwasaidia kwa taratibu za kisheria”.
IOM nchini Libya Jumatatu ilisema itatoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa wahamiaji waliookolewa kwenye mpaka na Tunisia.