Sera tata ya serikali ya Uingereza kusitisha mtiririko wa wahamiaji inakabiliwa na changamoto kali zaidi wiki hii wakati Mahakama ya juu ya Uingereza ikipima kama ni halali kuwapeleka wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda.
Serikali ya kihafidhina inapinga uamuzi wa mahakama ya rufaa ya mwezi Juni ambayo ilisema sera iliyo afikiwa ya kuwazuia wahamiaji kuhatarisha maisha yao kuvuka mfereji wa Uingereza kwa boti ndogo ni kinyume cha sheria kwa sababu nchi hiyo ya Afrika Mashariki si mahali salama pa kuwapeleka.
Siku tatu za kutoa hoja zimepangwa kuanza leo Jumatatu huku serikali ikisema sera yake iko salama na mawakili wa wahamiaji kutoka Vietnam, Syria, Iraq, Iran na Sudan wakidai kuwa ni kinyume cha sheria na kukiuka misingi ya utu.