Maafisa wanasema kuwa wenzano waliouwawa ni wa kutoka idara ya polisi ya eneo hilo na kwamba walikuwa wamelala pale wenzao watatu walipo wapiga risasi na kisha kutoroka na silaha zao.
Maafisa wa usalama kusini mwa Afghanistan wamesema takriban maafisa 7 wa polisi wameuwawa kwenye shambulizi linaloshukiwa kupangwa na mmoja wao kwenye jimbo la kusini la Kandahar.
Tukio hilo limefanyika mapema leo kwenye kituo cha usalama katika wilaya ya Arghandab. Maafisa wanasema kuwa wenzano waliouwawa ni wa kutoka idara ya polisi ya eneo hilo na kwamba walikuwa wamelala pale wenzao watatu walipo wapiga risasi na kisha kutoroka na silaha zao.
Msemaji wa Taliban amedai kuwa kundi lake limehusuka na shambulizi hilo akiongeza kusema maafisa waliotoroka wamejiunga na kundi hilo. Mamlaka ya Jimbo yameanza uchunguzi huko Kandahar karibu na mpaka wa Pakistan.