Shambulizi hilo la anga karibu na mji wa pwani wa Tyre limetokea wakati kuna ongezeko la juhudi za kimataifa za kidiplomasia, kuzuia mgogoro kati ya Hezbollah na jeshi la Israel kuongezeka na kuwa vita ambavyo vinaweza kusababisha mgogoro wa moja kwa moja kati ya Israel na Iran.
Taarifa ya Hezbollah imemtaja kamanda aliyeuawa kuwa Mohammad Naameh Nasser, anayejulikana kwa jina Abu Naameh.
Naameh ni afisa wa juu sana wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, kuuawa tangu kifo cha Taleb Sami Abdullah, aliyeuawa katika shambulizi la anga la Juni 11.
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, amemtaja Abdullah kuwa mtu muhimu katika kundi hilo tangu mapambano yalipoanza Oktoba 8, akiongoza kikundi cha Nasr.