Shambulizi huko Libya limepiga nyumba ya Ibrahim Dbeibah; inasema Al Wasat TV

Ramani ya Libya na nchi zilizo jirani nao.

Ikinukuu chanzo cha usalama kisichojulikana, kituo hicho kilisema Ibrahim Dbeibah hakuwepo nyumbani wakati roketi hizo zilipopiga

Shambulio lililolenga nyumba na ofisi ya mpwa wa Waziri Mkuu wa Libya mjini Tripoli halikusababisha vifo, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti Jumatatu.

Kituo cha televisheni cha Libya cha Al-Wasat kimesema moja ya makazi ya Ibrahim Dbeibah, ambaye pia ni mshauri wa mjomba wake, Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah yaliharibiwa Jumapili na maguruneti mawili yaliyorushwa kwa roketi.

Ikinukuu chanzo cha usalama kisichojulikana, kituo hicho kilisema Ibrahim Dbeibah hakuwepo nyumbani wakati roketi hizo mbili zilipopiga ofisi yake na paa la nyumba yake karibu na kitongoji cha makazi ya mji mkuu wa Libya, Hay Al-Andalus.

Kitengo cha Brigedi 166, chenye silaha ambacho kinahusika na usalama wa eneo hilo, mara moja kilifunga barabara na kuwaita wafanyakazi wa zima moto, kilisema chanzo cha usalama.

Milipuko miwili mikubwa iliyofuatiwa na milio ya risasi na ving'ora vya polisi, vilisikika Jumapili jioni wakati mashambulizi hayo yaliporipotiwa, mkazi mmoja akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, aliliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.