Serikali ya Uingereza yashinda pingamizi la wanaharakati

Waandamanaji wakiandamana nje ya Mahakama ya haki Uingereza huku kesi ya kisheria ikisikilizwa kuhusu kusitisha mpango wa kuwafukuza waomba hifadhi kutoka Uingereza hadi Rwanda.Ijumaa Juni 10,2022.(AP/Frank Augstein).

Serikali ya Uingereza ilishinda pingamizi la kisheria kwa sera yake tata ya kuanza kuwafukuza waomba hifadhi nchini Rwanda huku Mahakama Kuu ikitupilia mbali majaribio ya wanaharakati ya kutaka kushinda amri ya kizuizi  na kusema kwamba ndege ya kwanza inaweza kuondoka wiki ijayo.

Mashirika ya kutoa misaada na chama cha wafanyakazi walikuwa wameanzisha changamoto mapema wiki hii dhidi ya mpango huo wa serikali wa kutuma waomba hifadhi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Jaji Jonathan Swift siku ya Ijumaa alikataa kuzuia kuondolewa kwa waomba hifadhi wa Iraq na Syria na akaondoa amri ya kuzuia safari ya kwanza ya ndege kuelekea Rwanda siku ya Jumanne.