Marufuku ya kusafiri ilitangazwa Jumatatu na kuwalenga maafisa ambao hawakutajwa ambao Marekani inahisi wanawajibika katika kuhujumu demokrasia na kukandamiza watu wa tabaka la wachache nchini Uganda, ikiwa ni pamoja na jamii ya LGBT. Uganda ilipitisha moja wapo ya sheria kali kabisa duniani dhidi ya wapenzi wa jinsia moja mwezi Mei ambayo inahitaji adhabu ya kifo miongoni mwa mambo mengine, kwa vitendo vya ushoga.
Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Okello Oryem ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kuna njama ya mapinduzi inayofanywa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambayo anasema inaongozwa na watu wanaohimiza ajenda ya jamii ya LGBT Afrika.
Oryem anahoji, “kwanini wasipitishe vikwazo kama hivyo katika nchi za Mashariki ya Kati ambazo zina sheria sawa au hata kali dhidi ya LGBT? “Ikiwa wanakata kuwapiatia visa wabunge wetu, basi watakwenda Shangai, Guangzhou, na kuna maeneo mengine mengi mazuri kutembelea”
Marekani iliweka duru ya kwanza ya marufuku kwa maafisa wa Uganda kujibu sheria mwezi June na Benki Kuu ya Dunia ilisitisha mikopo kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwezi Ogusti.