Serikali ya Tanzania tayari kwa majadiliano ya katiba

  • Dinah Chahali

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Mungano ya Tanzania Mizengo Pinda amesema yuko tayari kuzungumza na kushauriana na rais juu ya njia bora ya kushirikisha makundi muhimu katika jamii ya jinsi ya kushughulikia suala hilo ya mabadiliko ya katiba.

Bw Pinda alikua anazungumza na waharirir wa habari mjini Dar es Salaam siku ya Ijumaa wakati shinikizo juu ya katiba mpya limeshika kasi nchini humo.

Anasema "nigetaka kusema kwamba mimi ninadhani kama serikali, isije watu wakapata hisia kwamba kuna kigugumizi kuna ugumu, hapana hakuna ugumu hata kidogo. Mimi ninadhani ni jambo ambalo limefika mahali linaonekana sasa limeiva watu wakae chini walizungumze tuone njia bora kuendelea mbele".

Mbali na suala la mjadala juu ya katiba, wazir mkuu Pinda alizungumzia juu ya mahakama ya kadhi, suala la umeme, pamoja na mikakati ya utendaji wa kazi na kilimo.