Serekali ya Somalia Alhamisi imesema wanajeshi wake wanaoungwa mkono na washirika wake wa kimataifa, na wanamgambo wa kikoo wamewaua takriban wanamgambo 350 wa Al Shabab na kujeruhi dazeni zaidi katika oparesheni tofauti katika maeneo ya kusini na kati.
VOA haikufanikiwa kuthibitisha ripoti za idadi ya vifo na hakukuwa na majibu ya haraka kutoka kwa kundi la Al Shabab kupitia msemaji ama mtandao wake.
Kwa mujibu wa maafisa wa Somalia, jeshi la kitaifa la Somalia lilifanya oparesheni mjini Hiraan katika jimbo la Hirshabelle, Mudug jimboni Galmudug, na eneo la Iower Jubba katika jimbo la Jubaland.
Katika mkutano na wanahabari mjini Mogadishu, Alhamisi, naibu waziri wa habari wa Somalia, Abdirahman Yusuf Adala amesema katika eneo moja la Hirshabelle zaidi ya wanamgambo 200 wa Al Shabab waliuwawa.