Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike Februari 25, ulicheleweshwa na tarehe mpya bado haijatangazwa.
Baraza la katiba lilibadilisha mswaada uliotaka uchaguzi kucheleweshwa hadi mwezi Desemba, hatua ambayo ilipelekea vurugu na hasira katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.
Rais wa Senegal Macky Sall, ambaye alisema kwamba kucheleweshwa kwa uchaguzi ni hatua iliyochukuliwa kutokana na kutokubaliana kuhusu orodha ya wagombea, ameahidi kuheshimu maamuzi ya mahakama na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuandaa uchaguzi haraka iwezekanavyo.
Orodha mpya ina wagombea 19 wa urais baada ya Rose Wardini kujiondoa kwenye kinyang’anyiro.
Wanasaisa maarufu wa upinzani Ousmane Sonko na Karim Wade, mtoto wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade, hawajajumuishwa kwenye orodha ya wagombea wa urais.