Serikali ya Rais Nicolas Maduro iliongeza mbinu za ukandamizaji za kuyavunja maandamano ya amani na kuendeleza madaraka baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata nchini Venezuela mwezi Julai, ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema Jumanne.
Mamlaka za uchaguzi zilimpatia Maduro ushindi huo, bila kuonyesha hesabu ya matokeo ya kura, lakini upinzani ulisema mgombea wake Edmundo Gonzalez alishinda kwa kishindo, hesabu yakura ikithibitisha hilo. Zaidi ya darzeni mbili ya watu waliuawa katika maandamano huku wengine 2,400 walikamatwa.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaotafuta ukweli, ambao uliwahoji watu mia kadhaa kwenye maeneo mbali-mbali au katika nchi nyingine, kwa kuwa ulinyimwa fursa ya kuingia Venezuela, umesema mamlaka zilijaribu kuuvunja upinzani, kuzuia taarifa huru, na kuzuia maandamano.