Baadhi ya wanaharakati waliwataka watu kukusanyika siku ya Alhamisi wakiwa na vifaa vya kupigia kambi ili kukaa katika bustani ya Uhuru iliyo karibu na katikati mwa jiji, huku kukiwa na wingi wa polisi kote Nairobi.
Watu wasiopungua 50 wameuawa katika maandamano yaliyoongozwa na vijana kupinga mapendekezo ya nyongeza ya kodi yaliyozuka kote nchini Kenya mwezi mmoja uliopita na yameendelea hata baada ya Rais William Ruto kuondoa muswaada wa sheria hiyo na kuwafuta kazi takriban baraza lake lote la mawaziri.
Wanasema wanataka Ruto ajiuzulu na wanataka mageuzi yafanyike ili kuondoa ufisadi na kushughulikia utawala mbovu.