Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya, Profesa Halim Shauri ameikosoa serikali ya Kenya kwa madai ya kushindwa kuangalia maslahi ya vijana hali inayodaiwa kuchangia vijana wengi kujiunga na makundi ya uhalifu pamoja na makundi ya kigaidi.
Your browser doesn’t support HTML5
Profesa Shauri aliitaka serikali ya Kenya kubuni nafasi za ajira ili kuweza kuwanusuru vijana wenye nia ya kujiunga na makundi hayo ya magenge ya uhalifu uliotukuka. “wengine wamesema kwamba watapea vijana kazi kupitia ile sijui inaitwa NYS, lakini kazi yenyewe iko wapi kwa hivyo ni lazima serikali ijizatiti na iwajibike katika kupeana ajira kwa vijana ili vijana waweze kuacha kushawishiwa kwa kupewa ajira ambazo sio nzuri ambazo zinatuletea balaa extremism na radicalization katika nchi yetu”.
Msomi huyo alishikilia kwamba ni sharti serikali imwangazie kijana ili aweze kujiinua kiuchumi na sio kutumiwa nyakati za kisiasa.