Serikali ya Botswana ilieleza kwamba itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu nchini humo ambao uliondoa sheria ya kuwahukumu mashoga na kukiuka sheria ambayo ilitoa adhabu kwa watu wa mapenzi ya jinsia moja kwenda jela hadi miaka saba.
Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa mwezi Juni mwaka huu ambao ulisifiwa na taasisi za kimataifa pamoja na wanaharakati wanaotetea haki za mashoga uliomaanisha kwamba Botswana ni moja ya nchi za kiafrika ambayo inaidhinisha mahusiano ya jinsia moja.
Mwanasheria mkuu nchini Botswana, Abraham Keetshabe alieleza katika taarifa iliyotolewa Ijumaa jioni kwamba mahakama kuu ilikosea kutoa uamuzi wake na kurudi kwenye sheria za enzi ya ukoloni.